Ruka hadi kwenye maudhui makuu
ZIMBABWE KUSHUHUDUA DEMOKRASIA MPYA BAADA YA DICTATOR MUGABE KUBWAGA MANYANGA.
Kiongozi mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema nchi yake kwa inashuhudia mwanzo wa demokrasia mpya.
Mnangagwa,
ambaye anatarajia kuapishwa kushika wadhfa wa Urais wa nchi hiyo siku
ya Ijumaa, amesema kipaumbele chake ni kujenga upya uchumi wa nchi hiyo
na kuunda ajira mpya kwa idadi ubwa ya watu wasio na ajira.
Katika
hotuba yake hiyo, aliyokolezwa na maneno yaliyokuwa yakitumika wakati
wa vita vya uhuru wa nchi hiyo, Bwana Mnangagwa alilishukuru jeshi la
nchi hiyo, ambalo liliingilia kati baada ya yeye kufukuzwa na Rais
Robert Mugabe na kuweza kufanikisha hali iliyopo sasa kwa amani.
Makamu huyo wa Rais wa zamani anayesubiri kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo alirejea nchini Zimbabwe mapema jana.
Aidha alifahamisha kuwa aliikimbia nchi hiyo baada ya kutishiwa maisha yake baada ya kufukuzwa katika nafasi yake hiyo.
Maoni
Chapisha Maoni