ZITTO KABWE KUFUNGUA KESI YA KIKATIBA DHIDI YA JESHI LA POLISI KWA KUSHIKILIA SIMU YAKE
Pata kiungo
Facebook
X
Pinterest
Barua pepe
Programu Nyingine
Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe, amesema anajipanga kulifungulia
kesi ya kikatiba jeshi la polisi nchini kutokana na kushikilia simu
yake.
Zitto ameeleza kuwa simu yake inashikiliwa tangu Novemba 7 mwaka huu
alipokamatwa kwa tuhuma za kuvunja sheria ya takwimu na sheria ya
makosa ya mtandao.
“Walisema watahitaji simu hiyo kwa siku mbili tu, nilikwenda polisi
KAMATA siku tatu baadaye nikaelezwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi.
Nimerudi leo tarehe 20, Polisi wanasema bado wanahitaji simu yangu
hiyo”, amesema Zitto.
==>Aliyoyasema Zitto kupitia akaunti yake ya Facebook:
Ndugu, Jamaa na Marafiki, mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 7/11/2017 Jeshi
la Polisi walichukua Simu yangu kwa ajili ya uchunguzi wao kuhusu tuhuma
dhidi yangu kwa mujibu wa sheria ya takwimu na sheria ya makosa ya
mtandao. Walisema watahitaji simu hiyo kwa siku 2 tu.
Nilikwenda polisi KAMATA siku 3 baadaye nikaelezwa kuwa bado wanaendelea
na uchunguzi. Nimerudi leo tarehe 20/11/2017, Polisi wanasema bado
wanahitaji simu yangu hiyo.
1) Nawakumbusha kuwa msitumie simu ile 0767777797 kwani bado imeshikiliwa na Polisi
2) Katiba ya Nchi yetu kifungu cha 16(1) na (2) imeweka msingi wa nguvu
sana haki ya FARAGHA kwa raia na kwamba hata sheria ikitaka haipaswi
kuingilia mawasiliano binafsi ya Raia.
Nina mashaka kuwa Jeshi la Polisi linakaa na Simu yangu muda wote huu
kwa sababu za zaidi ya uchunguzi wao wa makosa wanayonituhumu nayo.
Nimeamua kuwaachia Simu mpaka hapo watakapotosheka lakini wajiandae na
kesi ya kikatiba ambayo pia italinda haki za wananchi wengi wanaothirika
na matumizi mabaya ya sheria ya Mtandao ( cybercrime act ).
Maoni
Chapisha Maoni