Kamati ya Utendaji ya Baraza la Vijana
wa Chadema (Bavicha) limemchagua Patrick Ole Sosopi kuwa Mwenyekiti wa
baraza hilo kuchukua nafasi ya Patrobasi Katambi aliyehamia Chama cha
Mapinduzi.
Kamati hiyo pia leo Desemba 2 imetangaza kuziba nafasi ya nafasi ya
Makamu Mwenyekiti kwa kumteua John Pambalu, nafasi iliyoachwa wazi na
Sosopi. Viongozi hao wameteuliwa kuongoza baraza hilo kwa muda wa mwaka
mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita
amesema uamuzi huo ulifanyika jana kufuatia kikao cha dharura cha kamati
hiyo ya utendaji.
Amesema baraza hilo ni mojawapo ya taasisi imara na itaendeleza
mapambano."Tunawahimiza vijana wa Chadema na vijana wote wa Tanzania
wasimame kidete kwenye kazi ya kuijengea na kuipigania demokrasia ya
nchi yetu katika misingi ya utawala bora na haki za binadamu,"
Kwa upande wake Ole Sosopi amesema katika uongozi wake atahakikisha
baraza hilo linarudi kwenye misingi imara na kuongoza mapambano ya kudai
demokrasia.
Amesema akiwa mwenyekiti hatavumilia kuendelea kuona uonevu wanaofanyiwa wanachama wa Chadema.
"Bavicha inaenda kuwa taasisi bora na imara zaidi baada ya kuondoka
Katambi. Tunakwenda kupambania Demokrasia a, tutawashawishi vijana kuwa
wamoja kulitetea taifa bila kujali maslahi ya vyama," amesema Ole Sosopi
Maoni
Chapisha Maoni