SABABU ZA MAULID MTULIA KUJIUZULU UBUNGE NA UANACHAMA CUF NA KUHAMIA CCM WATANZANI WAENDELEA KUWASHANGAA WANAONUNULIWA.
Mbunge wa Kinondoni jijini Dar, Maulid
Mtulia (CUF) ametangaza kujiuzulu ubunge na kujivua uanachama wa Chama
cha Wananchi CUF na kuhamia CCM.
Katika barua yake ya kujiuzulu, Mtulia amesema kuwa ameamua kufanya
uamuzi huo Disemba 2,2017 kwa utashi wake bila shinikizo la mtu yeyote.
Mtulia ameelezea sababu za kujiuzulu nafasi yake hiyo ya ubunge na
kuhama chama kuwa imetokana na uzoefu alioupata kwa miaka miwili ya
ubunge, na kusema “nimebaini kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
ambacho ni chama tawala inafanya kazi kubwa ya kutekeleza Ilani na
imefanya vizuri katika mambo mengi ambayo sisi upinzani tuliahidi
kuyatekeleza” alisema.
Aidha Mbunge huyo amesema kuwa nia yake ni kuwatumikia wananchi, na
haoni sababu ya kuendelea kuwa upinzani na badala yake anaona ni vema
aungane na juhudi za Serikali, kwa kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli
katika kuwaletea wananchi maendeleo na kukabiliana na kero mbalimbali.
Maoni
Chapisha Maoni