WABUNGE WA CHADEMA, MADIWANI NA WANACHAMA WA CHADEMA WAENDELEA KUSOTA RUMANDE.

 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro, imewanyima dhamana wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Lijualikali, Suzan Kiwanga na wafuasi wengine 34 wa Chama hicho wakiwepo madiwani, kwa kuwarudishwa mahabusu hadi Disemba 04 mwaka huu.

Wabunge hao walikamatwa mapema wiki hii kwa tuhuma za kufanya vurugu katika uchaguzi wa madiwani ikiwa ni pamoja na kuchoma moto shule na rasilimali nyingine za umma.

Aidha, Polisi wa mkoani Morogoro iliwatia mbaroni watu 41 akiwemo mbunge wa Mlimba (Chadema), Susan Kiwanga, madiwani wawili kwa madai ya kufanya fujo na kuchoma moto majengo ya shule baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Sofia.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi, Ulrch Matei amesema kuwa viongozi hao walikuwa wakiwachochea wafuasi wa chama hicho kuchoma moto nyumba ya walimu wa shule ya Sofi na ofisi ya mtendaji kata na pia hata baada ya kuchoma majengo hayo kwa kutumia petroli, walidhamiria pia kwenda katika zahanati lakini askari waliwakamata, huku Peter Lijualikali akijisalimisha mwenyewe.

Maoni